Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.
Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imefanikiwa sana kuongeza ukaribu na
wananchi kwa kusikiliza changamoto na kuzitatua kwa haraka kupitia Mfumo wa
Sema na Rais Mwinyi (SNR).
Rais Dk. Mwinyi amesema mfumo wa SNR ni kiungo muhimu kati ya
Serikali na wananchi pia ni kigezo cha utawala bora unaozingatia ushirikishwaji
wa wananchi.
Rais Dk. Mwinyi amesema hayo katika hafla ya Maadhimisho ya
Miaka 3 ya Mfumo wa Sema na Rais Mwinyi (SNR) tarehe: 16 Machi 2024 katika
Viwanja vya Ikulu Mnazi Mmoja.
Aidha, Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa kitengo cha SNR kina
wajibu kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kutumia njia mbalimbali kwa wananchi
ili waweze kutumia vema Mfumo huu kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
Kwa upande mwingine Rais Dk. Mwinyi amesema katika kipindi
cha Miaka 3 tangu kuanzishwa kwa Mfumo wa SNR jumla la malalamiko 13,517
yamepokelewa kati ya hayo 11,116 yamepatiwa ufumbuzi na 2,351 yanaendelea
kufanyiwa kazi katika hatua mbalimbali.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyombo vya ulinzi na usalama
na Vyama vya Siasa wamehudhuria hafla hiyo.
0 Maoni