Mgombea wa upinzani kijana ashinda urais wa Senegal

 

Bassirou Diamaye Faye (44) ameshinda kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa Senegal siku chache tu, tangu aachiwe kutoka gerezani.

Mgombea huyo ambaye anaelekea kuwa rais kijana kuliko wote Afrika, alikuwa hajulikani kabisa mwaka mmoja uliopita.

Amadou Ba wa chama tawala amekiri kushindwa na Faye na kumtumia pongezi hata kabla ya matokeo ya jumla kutangazwa.

Kwa hali inavyoonekana ni dhahiri hakutakuwa na uchaguzi wa marudio kutokana na idadi ya kura alizopata Faye.

Chapisha Maoni

0 Maoni