Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza benki ya NMB kwa
kuiunga mkono Serikali kwa kuisaidia jamii ikiwemo watoto wanaoishi katika
mazingira magumu.
“Kwa kufanya hivi mnapata thawabu kwa kuyagusa maisha ya
jamii yenye uhitaji na kuwafanya wajione wenye thamani sawa na wengine.
Ninatambua kuwa licha ya kuwakumbuka Watoto wenye uhitaji, mmekuwa mkichangia
mahitaji muhimu kwenye shule mbalimbali nchini.”
Amesema hayo leo (Jumanne, Machi 26, 2024) aliposhiriki
katika Iftari na watoto wanaoishi katika mazingira magumu, viongozi mbalimbali
wa Serikali na Wafanyakazi wa NMB.
Kadhalika Mheshimiwa Waziri Mkuu aliipongeza benki hiyo kwa
kuunga mkono mipango na mikakati mbalimbali ya Serikali ikiwemo kwa kuwa na
dirisha la Kilimo ambalo limetoa mikopo wa shilingi trilioni 1 kwa wakulima.
“Ninaipongeza sana Benki ya NMB kwa kutoa gawio la shilingi
bilioni 45.5 Serikali kwa Serikali kwa mwaka 2023.”
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dkt. Edwin Mhede amesema kuwa matukio kama haya yanalenga kujenga jamii ya watu wenye hofu na Mungu katika kukuza uchumi wa nchi na kusimamia taasisi zinazojielekeza na masuala ya fedha.
0 Maoni