Treni ya SGR yafanya majaribio ya kwanza ikiwa na mabehewa

 

Shirika la Reli Tanzania (TRC), leo limefanya majaribio ya treni ya kisasa ya SGR kwa mara ya kwanza ikiwa na mabehewa kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro.

Mkrurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa amesema majaribio hayo yamefanyika baada ya kufanywa majaribio kadhaa ya awali ya vichwa vya treni ya SGR kwa mafanikio.

Amesema majaribio hayo ni mwendelezo wa majaribio menginea kadhaa yatakayofanywa ili kuhakikisha kila kitu kinafanyakazi kwa ufanisi.

“Wataalamu wetu wanafanya majaribio ya vitu vingi ambavyo vinapimwa utendaji wake, nyie mnao ona mnaiona treni lakini sisi tunapima vitu vingi sana,” amesema Kadogosa.

Bw. Kadogosa amesema safari hii wamefanya majaribio hayo wakiwashirikisha waandishi wa habari, ili waweze kufikisha habari kwa Watanzania kuhusiana na hatua iliyofikia mradi huo.

Chapisha Maoni

0 Maoni