Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi
Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima amesema, uimara na uwezo wa kiakili wa mtoto
hujengwa kuanzia mwaka sifuri mpaka miaka minane (0-8).
“Makuzi na uslama wa mtoto huanzia tangu akiwa tumboni mwa
mama yake. Yanategemea mama huyo ulimlisha nini, ulikuwa unazungumza naye nini
na hata baada ya kuzaliwa, mtoto ulimleaje? Hapa ndio tunapata watoto wenye
uwezo mkubwa baadaye na taifa linakuwa na wataalamu,” amesema Dk. Gwajima.
Ametoa kauli hiyo leo tarehe 26 Februari 2024, wakati
akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam, kuhusu
Mkutano wa Kimataifa wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto
utaofanyika tarehe 11 – 14, Machi 2024, jijini Dar es Salaam.
Dk. Gwajima amewaeleza wahariri kuwa, Rais Samia Suluhu
Hassan atakuwa mgeni rasmi na kwamba, utakuwa na ugeni mkubwa utakaojumuisha
washiriki zaidi ya 1,100 ambapo, kati yao washiriki 700 wanatoka nje ya
Tanzania ikijumuisha nchi za Afrika Mashariki, Afrika, Ulaya na Amerika na
zaidi ya washiriki 400 watatoka Tanzania.
“Nchi yetu imepata fursa ya kuandaa mkutano huo kutokana na
jitihada na mafanikio kadhaa yaliyopatikana katika kuandaa na kutekeleza
Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto
yaani JPT - MMMAM ya 2021/2022- 2025/2026,” amesema Dk. Gwajima.
Joseph Kulangwa, Mhariri wa Gazeti la Raia Mwema ameishauri serikali kuwa makini na baadhi ya nyumba za ibada ambazo zimekuwa zikiyumbisha makuzi ya watoto.
“Kuna Kanisa liligomea watoto kupata chanjo, chanjo ni
sehemu ya usalama wa mtoto. Sasa makanisa kama haya yanaweza kutupeleka siko,”
alisema Dk. Gwajima.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania
(TEF), Angela Akilimali ameeleza matarajio ya Watanzani akutokana na mkutano
huo.
Hata hivyo ameishukuru serikali kwa juhudu zilizopelekea kupata wasaa wa kuandaa mkutano huo na kwamba, utakuwa na matokeo chanya kwa taifa.
0 Maoni