Saratani yachukua uhai wa Rais Hage wa Namibia

 

Rais wa Namibia Hage Geingob amefariki dunia akipatiwa matibabu kwenye hospitali moja ya Jiji la nchi hiyo la Windhoek.

Makamu wa Rais Nangolo Mbumba ametangaza kuwa rais Geingob amefariki dunia mapema leo Jumapili majira ya asubuhi.

“Wakati akiaga dunia, alikuwapo mkewe Madame Monica Geingob pamoja na watoto wake,” imesema taarifa ya Bw. Mbumba.

Kiongozi huyo wa nchi mwenye umri wa miaka 82 alibainika kuugua Saratani na aliuarifu umma kuwa na maradhi hayo mwezi uliopita.

Kwenye mtandao wa kijamii wa X, Rais Samia Suluhu Hassan, ameandika Rest in Peace my Dear Brother, Dr. Hage G. Geingob, President of the Republic of Namibia (Pumzika kwa Amani Kaka yangu Mpendwa Dkt. Hage G. Geingob, Rais wa Jamhuri ya Namibia).


Chapisha Maoni

0 Maoni