Meli yenye watalii zaidi ya 100 yatia nanga hifadhi ya magofu ya kale Kilwa Kisiwani

 

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA jana Februari 03, 2024 imepokea meli kubwa ya watalii wapatao 102 kutoka Uingereza waliofika katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara kwa ajili ya shughuli za utalii kisiwani humo.

Watalii hao wakiongozwa na Kampuni ya Utalii ya Takim Holidays walipokelewa na kukaribishwa kwa ngoma za asili ya watu wa Kilwa Kisiwani iitwayo kitupolo ambayo iliwafanya waonekane wakifurahi muda wote.

Ngome ya Mreno, Msikiti mkubwa na mkongwe, Makaburi ya Malindi na Makutani Palace ni miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa na watalii hao ikiwa ni pamoja na kupata fursa ya kujifunza tamaduni za watu wa Kilwa kisiwani.

Historia na upekee wa Hifadhi hii ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara imekuwa kivutio kikubwa cha watalii kutoka Kona mbalimbali za Dunia ambao hutembelea Hifadhi hiyo Karibu Kila Mwaka.

TAWA inatarajia kuendelea kupokea Meli nyingine zaidi katika kipindi cha Mwezi Februari na Machi, 2024, na hii yote ni kutokana na Kazi kubwa iliyofanywa na muongoza watalii "Tour Guide" namba moja Nchini Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Chapisha Maoni

0 Maoni