RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.
Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa wadau mbalimbali kutambua umuhimu wa
ushirikiano ili kufikia malengo kwa kuwekeza rasilimali fedha katika kuimarisha utafiti, kuboresha miundombinu ya
afya, na kuhakikisha upatikanaji matibabu sawa kwa wagonjwa wa saratani nchini.
Rais Dk. Mwinyi amesema hayo katika jukwaa la uwekezaji
linalolenga kuimarisha huduma za saratani nchini, ukumbi wa Hoteli ya Hyatt
Regency Dar es Salaam tarehe 06 Februari 2024.
Vilevile Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa kupitia ushirikiano
kati ya Serikali, sekta binafsi, watafiti na wataalamu wa tiba kunaweza
kubadilisha taswira za huduma za matibabu ya saratani nchini.
Aidha Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali imeanza kuchukua
hatua kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo saratani kwa kujenga
miundombinu ya huduma za afya, mikakati ya upatikanaji wa huduma bora za
matibabu bora kwa wote.
Halikadhalika Rais Dk. Mwinyi ameishukuru Serikali ya
Marekani kwa ushirikiano wao kufanikisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo
ikiwemo sekta ya afya nchini.
Pia amewashukuru wadau wa Global Health Catalyst ambao wamejitolea kushirikiana na Serikali
katika mapambano ya maradhi ya saratani, wawekezaji wa ndani wakiongozwa na
Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) pamoja na CEO Roundtable kwa utayari walionyesha
kushirikiana na Serikali.
Rais Dk. Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi na jitihada zake za kuimarisha ustawi wa maendeleo nchini.
0 Maoni