Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.
Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali za sekta ya
utalii ikiwemo ajira, kuuza mazao wanayozalishwa nchini na usafirishaji.
Rais Dk. Mwinyi amesema hayo alipofungua Mkutano wa pili wa
Kimataifa wa sekta ya utalii na Maonesho "The Z Summit 2024" katika
ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, uwanja wa ndege Zanzibar tarehe: 21 Februari
2024.
Aidha Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali itaendelea kujenga
miundombinu ya ujenzi wa barabara mpya, kuboresha usambazaji wa umeme na maji
pamoja na viwanja vya ndege.
Halikadhalika, Rais Dk. Mwinyi amesema Sheria mpya ya
uwekezaji Zanzibar ya mwaka 2024 imeweka vivutio vingi ambavyo vinalinda uwekezaji
na kuwa vivutio vya kodi Afrika Mashariki.
Kwa upande mwingine Rais Dk. Mwinyi amesema Pemba ni chachu ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya baadae kwa kuanzishwa ukanda wa uwekezaji wa Pemba (PIZ) ili kuvutia wawekezaji na kuchochea shughuli za kiuchumi.
0 Maoni