Wakina mama wa Hanang wahamasika kuchunguzwa Saratani

 

Wakina mama wakazi wa Wilaya ya Hanang wameonesha kuhamasika mno katika kujitokeza kuchunguzwa Saratani ya Shingo ya Kizazi pamoja na Saratani ya Matiti katika zoezi linaloratibiwa na Wizara ya Afya pamoja na USAID.

Kila inapofika mwezi Januari Tanzania huungana na ataifa mengine duniani kuhamasisha huduma za uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi, akina Mama Wilayani Hanang Mkoani Manyara wamekuwa na mwitikio wa kuchunguza Saratani kutokana Elimu ya Afya inayotolewa.

Katika zoezi hilo, jumla ya akina mama 228 wamechunguzwa Saratani ya Mlango wa kizazi na matiti Wilayani Hanang, huku wataalamu wa afya wakitoa wito kwa wananchi kujenga tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara.

Baada ya kufanyiwa vipimo wakina mama hao, wamama watatu wamegundulika kuwa na maambukizi ya Saratani ambapo, mmoja wao alikuwa na Saratani ya mlango wa kizazi na alipewa rufaa ya kwenda Hosipitali ya Hydom.

 Wizara ya Afya kupitia Idara ya Afya ya Uzazi Mama na Mtoto ikiambatana na wadau wa maendeleo USAID afya yangu Kaskazini, imetumia fursa ya uhamasishaji  mwezi huu kuhusu ugonjwa wa Saratani ya mlango wa  kizazi kuwatia moyo wakazi wa Hanang waliokumbwa na maafa ya mafuriko kwa kufikisha huduma hii karibu ya uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi.

Chapisha Maoni

0 Maoni