Umoja wa Ulaya watoa milioni 275 kwa waathirika Hanang

 

Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza msaada wa kibinadamu wa Euro 100,000 sawa na shilingi milioni 275 za Tanzania kuwasaidia watu walioathirikana maporomoko ya ardhi na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha Mlima Hanang na maeneo mengine ya Tanzania.

Fedha hizo zitatumika kulisaidia Shirika la Msalaba Mwekundu katika kutoa msaada wa kujikimu na kuimarisha kaya 44,000 kwenye mikoa iliyoathirika zaidi ya Manayara, Dar es Salaam, Kigoma, Kagera, Geita pamoja na Unguja.

Msaada huyo utakuwa ni wa utaoaji wa chakula, maji, usafi wa mazingira na mwili, hifadhi, afya pamoja na huduma za ulinzi wa kaya zilizoathiriwa na maafa ya maporomoko ya ardhi na mafuriko kwenye mikoa tajwa.

Katika taarifa yao hiyo iliyotolewa leo Umoja wa Ulaya umesema utaendelea kuwa pamoja na watu wa Tanzania katika kipindi hiki kigumu, na umejidhatiti katika kuwaunga mkono kuhakikisha wanayakabili majanga ya kibinadamu na kurejea katika maisha ya kawaida.

Chapisha Maoni

0 Maoni