Rais Samia atuma salamu za pole vifo vya wachimbaji 21

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kufuatia kutokea vifo vya wachimbaji madini wadogo 21 katika ajali ya kufunikwa na ardhi kwenye mgodi wa Ng'alita, Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa X Rais Samia ameandika “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu zaidi ya 21 kufuatia ajali ya kufunikwa na ardhi katika Mgodi wa Ng'alita, Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu. Ndugu zetu hawa walikuwa wachimbaji wadogo katika eneo hili, wakijitafutia riziki zao, familia zao na kuchangia maendeleo ya taifa letu.”

Natuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza jamaa zao katika ajali hii. Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikishirikiana na uongozi wa mkoa vinaendelea na juhudi za kutafuta miili mingine ambayo bado imekwama ndani ya kifusi, imesema taarifa yake.

Chapisha Maoni

0 Maoni