Rais Dkt. Mwinyi akutana na Mwenezi Makonda Ikulu Zanzibar

 

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa Paul Christian Makonda, Ikulu Zanzibar tarehe 11 Januari 2024.

Aidha, Katibu Mwenezi Makonda amempongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa kazi nzuri anayoendelea kufanya kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 kipindi cha Miaka 3 kwa miradi mbalimbali ya maendeleo Zanzibar.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi  ampongeza Katibu Mwenezi Makonda kwa kuteuliwa kwake na kuanza kazi vizuri  ya ujenzi wa Chama cha Mapinduzi kwa umma.

Chapisha Maoni

0 Maoni