DED aahidi milioni 15 kwa Mwalimu Mkuu msingi atakayefaulisha

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Kiomon Kibamba amewaahidi walimu wakuu wa shule za msingi zitakazo faulisha wanafunzi wengi katika halmashauri hiyo, atawapatatia zawadi ya fedha shilingi milioni 15.

Kibamba amesema kwamba iwapo mwalimu akitaka atanunuliwa gari lenye thamani ya fedha hizo, Kibamba amesema hatua hiyo ni maana ya kutambua mchango wa walimu katika kukuza sekta ya elimu kwa kupambania ufaulu mzuri wa wanafunzi.

Akiongea na walimu wa shule za msingi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, Kibamba amefafanua kuwa zawadi hiyo ya shilingi milioni 15 kwa Mwalimu Mkuu itatolewa kwa shule itakayofaulisha kwa asilimia 95 ya wanafunzi wote kwa wastani wa alama 100.

Chapisha Maoni

0 Maoni