Baba amuua mtoto wa miezi mitano kwa kipigo

 

Baba mmoja anatafutwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita baada ya kumuua mtoto wake wa miezi mitano katika Mtaa wa Kilimahewa Wilayani Geita, baada ya kumpiga sehemu mbalimbali mwilini kwa kutumia mkanda na kiatu.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Safia Jongo, amesema mtoto huyo Leonard Kabilu aliuawa siku ya Alhamisi Januari 11, 2024 saa saba usiku wakati akiwa amelala huku chanzo cha tukio hilo kikidaiwa ni ugomvi wa kifamilia.

Baada ya kutenda tukio hilo, mtuhumiwa aitwae Kabilu Mayege (20) alitoroka na Jeshi la Polisi mkoani Geita linaendelea kumtafuta baba huyo, amesema Kamanda Jongo.

Chapisha Maoni

0 Maoni