Mkono wa pole wa sh milioni 1 kutolewa kwa kila mwili Hanang

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa maagizo kwa Serikali kugharamia mazishi yote ya waliofariki kwenye maporomoko ya matope ya Mlima Hanang na kutoa mkono wa pole wa shilingi milioni moja kwa kila mwili.

Maagizo hayo ya Rais yameelezwa leo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Mobhare Matinyi ambapo pia amesema hadi kufikia sasa miili iliyopatikana ni 87 na yote imeshatambuliwa na ndugu zao na kuchukuliwa kwa mazishi.

Ameeleza kuwa hadi sasa jumla ya majeruhi na wagonjwa waliopokelewa tangu maafa yatokee ni 139 lakini waliopo hospitalini hadi leo ni 30.


Chapisha Maoni

0 Maoni