Makamu Mwenyekiti wa CCM
Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali
Mwinyi amewashukuru viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kuthamini
kuandaa mkutano uliojumuisha Wanawake kutoka sehemu mbalimbali nchini ikiwemo mikoa
yote ya Tanzania bara.
Dk. Mwinyi amesema hayo
katika mkutano wa kumpongeza kutimiza miaka mitatu ya uongozi wake ulioandaliwa
na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika viwanja vya Maisara Mkoa wa
Mjini Magharibi leo tarehe 04 Novemba 2023.
Aidha, Makamu Mwenyekiti wa
CCM Tanzania bara Abdulrahman Kinana ampongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kuimarisha
umoja, mshikamano na utulivu wa nchi na kuwaletea maendeleo Wazanzibari.
Amesema katika miaka miwili
iliyobaki utekelezaji wa miradi maendeleo utakuwa mkubwa zaidi na Zanzibar
baada ya miaka 10 itakuwa ya maendeleo makubwa.
Naye, Mwenyekiti wa UWT
Taifa Mary Chatanda amesema UWT wameridhika na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi
ya mwaka 2020/2025 kwa kuvuka malengo ya utekelezaji ndani ya miaka mitatu kwa
miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa Zanzibar.
Vilevile ameeleza kuwa UWT
watamchukulia na kumjazia fomu ya kuomba Urais wa Zanzibar Dk. Mwinyi pia
watafanya hivyohivyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Samia
Suluhu Hassan mwaka 2025.
0 Maoni