Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Mhe Albert Chalamila amepokea msaada wa vifaa tiba
vya thamani ya Milioni 137 kutoka katika Familia ya GSM vifaa tiba ambavyo
vimeelekezwa katika Taasisi ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam.
Siku hiyo ya leo (jana) imekuwa
muhimu na maalum kwa familia ya mmiliki wa GSM Bwana Gharib Mohamed ndio siku
aliyo zaliwa ambapo ameitumia siku hiyo kama Kumbukizi ya kuzaliwa kwake kutoa
msaada wa vifaa tiba katika Taasisi ya Ocean Road.
Akipokea msaada huo jana RC
Chalamila amesema kwa hatua aliyofikia Bwana Gharib Mohamed anachohitaji sasa
ni Mungu na Afya njema, "mwezetu GSM ameona ni busara wakati wa kumbukizi
ya siku yake ya kuzaliwa afanye jambo jema kwa wenye uhitaji hususani wagonjwa
wa cancer katika Taasisi ya ocean road, cha kujiuliza Je? wewe unapofanya
Kumbukizi ya kuzaliwa unafanya nini kwa wenye uhitaji," alisema Chalamila.
Aidha, RC Chalamila ametoa
rai kwa matajiri wote katika Mkoa wa Dar es Salaam kumheshimisha Mhe Rais Dkt
Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono juhudi mbalimbali za kuleta maendeleo
Katika Jamii. " Dkt samia Suluhu Hassan amekuwa akiwekeza sana katika
sekta ya Afya kwa kutambua umuhimu wake hata hivyo tayari ameshaidhinisha ununuzi
wa mashine ya kisasa katika Taasisi ya ocean road ambayo muda si mrefu itaanza
kutoa huduma," alisisitiza Mhe Chalamila.
Kwa upande wa Dkt Julius
Mwaisilage wa Ocean road amesema msaada wa vifaa tiba hivyo umekuja muda
muafaka kutokana na uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo katika Taasisi ya Ocean Road
hivyo amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuvisimamia vizuri vifaa hivyo ili viweze
kutoa huduma katika hali ya ubora kwa kipindi kirefu.
Mwisho RC Chalamila amesema fedha
hupotea lakini matendo hudumu alichokifanya Bwana Gharib Mohamed na familia
yake kitaendelea kudumu aidha ifahamike kuwa GSM ndiye mdhamini mkubwa wa timu
ya mpira Young African lakini hajaishia kwenye michezo tu ameendelea kuunga
mkono katika Sekta ya Afya hapa nchini.
0 Maoni