Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba uliofanyika mwezi
Septemba mwaka huu, huku likitangaza kufuta matokeo ya wanafunzi 31 kwa
udanganyifu.
Akitangaza matokeo hayo leo
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Said Mohamed amesema ufuaulu wa jumla umepanda
kwa asilimia 0.96 na kufikia asilimia 80.6 ambapo watahiniwa 1,092,960 wamefaulu
kwa daraja A, B na C.
Dk. Mohamed amesema kwa
jumla ya watahiniwa 1,397,395 walisajiliwa kufanya mtihani wa taifa wa darasa
la saba, ambapo wanawake ni 742,960 sawa na asilimia 53 na wanaume ni 654,603
sawa na asilimia 47.
Ameongeza kuwa hata hivyo ni
watahiniwa 1,356,397 tu ndio waliofanya mtihani wa taifa wa darasa la saba, ambapo
wanafunzi 40,901, hawakufanya mtihani huo uliofanyika Septemba 13-14, mwaka
huu.
Pamoja na mambo mengine Dk.
Mohamed amesema wanafunzi 360 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa
kufanya mitihani yote, au idadi kubwa ya masomo watarudia mitihani mwaka 2024.
Pata Matokeo Hayo Kwa Kutumia Link Hapo Chini :-
https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/index.htm
0 Maoni