Madudu yabainika kwenye makampuni binafsi ya ulinzi

 

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limebaini mapungufu katika kampuni binafsi za ulinzi ikiwemo walinzi kutokuwa na sifa ya kufanya kazi hiyo na wamiliki wa makampuni hayo kutopeleka makato ya michango ya watumishi wao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Zoezi la kukagua makampuni hayo binafsi katika wilaya ya Ilemela limeongozwa na Afisa Polisi Jamii mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Ramadhan Sarige pamoja na maafisa wengine wa jeshi hilo.

Kampuni zilizokaguliwa ni pamoja na West Security Serivices, Intelligence Securico na Masa Security Services Limited, mara baada ya kuzikagua ACP Sarige akawataka wamiliki wa kampuni zote za ulinzi kutoa ushirikiano na kuwasilisha nyaraka muhimu wakati wa ukaguzi huo.

"Nawaagiza wakuu wa Polisi wilaya OCD's na wakaguzi kata kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa kina kwa kuangalia nyaraka muhimu zinazotakiwa kuwepo kwenye kampuni binafsi za ulinzi na vitendea kazi vingine kwa mujibu wa sheria," amesema ACP Sarige.



Chapisha Maoni

0 Maoni