Kambi maalumu ya upasuaji wa kuweka nyonga na magoti bandia imeanza leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila.
Kambi hiyo inaendeshwa na Prof. Mamoun Gadir kutoka
Hospitali ya Queen Elizabeth ya nchini Uingereza, kwa kushirikiana na wataalamu
wa Mloganzila.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Upasuaji MNH-Mloganzila
Dkt. Godlove Mfuko amesema katika siku ya kwanza jumla ya wagonjwa sita
wamefanyiwa upasuaji na katika siku tano za kambi watu 35 watanufaika na
upasuaji huo.
Aidha, amebainisha kuwa kambi itaendelea hadi Desemba Mosi
mwaka huu na baada ya kambi utaratibu wa kawaida wa matibabu hayo utaendelea
ambapo wagonjwa wataendelea kuhudumiwa na wataalamu wazalendo.
0 Maoni