Waziri Kairuki aongoza Mkutano Mkuu wa 25 wa Shirika la Utalii Duniani

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki, (Mb), leo tarehe 18 Oktoba, 2023 ameongoza Mkutano Mkuu wa 25 wa UNWTO unaoendelea Jijini Samarkand, Uzbekistani.  Hatua hiyo imefuatia kuthibitishwa kwaTanzania na Nchi Wanachama kuwa Makamu wa Rais wa Mkutano huo.

Akiongoza Mkutano Mkuu wa UNWTO Mhe. Kairuki amezishukuru nchi wanachama wa UNWTO kwa kuichagua nchi ya Tanzania katika nafasi ya Makamu wa Rais na kuahidi kufanya kazi kwa karibu na nchi hizo ili kukuza na kuendeleza Sekta ya Utalii duniani.

Mkutano huo unaoendelea nchini Uzbekistani ulifungulia tarehe 16 Oktoba, 2023 na Rais wa Uzbekistan, Mheshimiwa Shavkat Mirziyoyev na unahudhuriwa na Mawaziri wa Utalii kutoka Nchi wanachama wa UNWTO zaidi ya 121 pamoja na Mashirika ya Kimataifa, Taasisi za kifedha na wadau kutoka sekta binafsi.

Chapisha Maoni

0 Maoni