Watu wapatao 1,100 wauawa Israel na Gaza

 

Watu wapatao 1,100 wameuawa Israel na Gaza tangu kuibuka kwa mapigano baina ya pande hizo mbili siku ya jumamosi.

Zaidi ya watu 700 wameuawa Israel tangu Hamas waanzishe mashambulizi yao na watu 400 wameuawa Gaza tangu Israel ianze kulipa kisasi.

Israel bado inapigana na wapiganaji wa Palestina katika maeneo saba hadi nane yaliyovamiwa na Hamas, jeshi la nchi hiyo limesema.

Israel imesema maeneo yote ya mpaka wake yanalindwa na vifaru, lakini haijakanusha uwezekano kuwa bado wapiganaji wa Hamas wanaingia Israel kutokea Gaza.

CHANZO: BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni