Salah ataka kuzingatiwa ubinadamu vita ya Isarel na Gaza

 

Mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah ametoa wito kwa viongozi duniani kuungana kuzuia mauaji zaidi ya watu wasio na hatia katika vita inayoendelea ya Israel na Gaza.

Maafisa wa afya wa Gaza wamesema mamia ya watu wameuawa katika shambulizi lililofanywa kwenye hospitali yenye watu wengi katika mji wa Gaza Jumanne usiku.

Salah mwenye umri wa miaka 31, amesema misaada ya kibinadamu kwenda Gaza lazima iruhusiwe mara moja.

“Kumekuwapo na ghazi nyingi, matukio ya kuvunja moyo na ukatili katika vita hiyo inayoendelea kati ya Isarel na Gaza,” amesema Salah.

Chapisha Maoni

0 Maoni