Rais Frank-Walter Stainmeier wa Ujerumani aanza ziara nchini

 

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu (3) kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi 1 Novemba 2023, na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba (Mb.) katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akikabidhiwa maua alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba (Mb.) wakati alipompokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akisalimian Balozi wa Ujerumani nchini Tanzani Mhe. Thomas Terstegen alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Ashatu Kijaji walikuwa miongoni mwa viongozi waliokuwepo kumpokea Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier.

Chapisha Maoni

0 Maoni