Moto wateketeza bweni shule ya Sekondari ya Omumwani

 

Moto umeteketeza bweni la wanafunzi katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Omumwani katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kagera, Zabron Muhumma, amesema kwamba tukio hilo limetokea jana majira ya saa 2:00 usiku.

Kamanda Mhumma amesema hata hivyo askari wa jeshi hilo walifanikiwa kuudhibiti moto huo kwa kushirikiana na wananchi na kuepusha kutokea madhara makubwa.

Moto huo umeteketeza mali, hata hivyo haukusababisha madhara yoyote kwa binadamu na hadi sasa chanzo chake hakijajulikana, amesema Kamanda Mhumma.

Chapisha Maoni

0 Maoni