Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya
wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam
Mwinyi ameshiriki katika shughuli ya ufungaji wa Jukwaa la nne la Viongozi
Wanawake lililoandaliwa na Mke wa Rais wa Burundi Mhe. Mama Angeline
Ndayishimiye.
Majadiliano na michango mbalimbali iliwasilishwa na
kujadiliwa katika Jukwaa hilo lililojikita kuelewa uwiano baina ya uzazi wa
Mpango Usalama wa Chakula, lishe na mgawanyiko wa faida ya kimahitaji kwa
makundi ya watu.
Waziri Mkuu wa Burundi Mhe.Gervais Ndirakubuca amefunga
rasmi jukwaa hilo jana katika ukumbi wa mikutano Hoteli ya Kiriri, Burundi.
Viongozi wanawake kutoka nchi mbalimbali wameshiriki wakiwemo
kutoka Kenya, Rwanda, pia wageni waalikwa mbali mbali wawakilishi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa Afrika na Kikanda pamoja na wadau wa maendeleo na ujumbe
kutoka China.
0 Maoni