Kenya kuongoza mapambano dhidi ya magenge Haiti

 

Umoja wa Mataifa umeunga mkono Kenya kuongoza vikosi vya mataifa mbalimbali nchini Haiti katika kuitikia wito wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuomba msaada wa kurejesha utulivu.

Haiti imekuwa ikikabiliwa na ghasi za magenge ya wahalifu, na ukatili unaoendelea sasa nchini humo umeshika kasi baada ya kuuawa kwa rais Jovenel Moïse Julai 2021.

Magenge ya wahalifu yametwaa mamlaka katika maeneo makubwa ya nchi hiyo, na kuwafanyia vitendo vya kigaidi wananchi na kuua mamia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, amesema kwamba matumizi ya nguvu yanahitajika kupokonya silaha magenge ya uhalifu ili kurejesha usalama.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limeridhia kupelekwa kikosi maalum kudhibiti magenge Haiti kwa muda wa mwaka mmoja, na kufanyiwa tathimini baada ya miezi tisa.

Chapisha Maoni

0 Maoni