Jeshi la Niger lazima mpango wa kutoroka Rais Bazoum

 

Serikali ya kijeshi ya Niger imesema imedhibiti jaribio la kutoroka nchini la aliyekuwa rais wa nchi hiyo aliyeondolewa madarakani Bw. Mohammed Bazoum.

Rais huyo wa zamani alijaribu kutoroka nchini usiku akiwa na familia yake, msemaji wa jeshi la Niger amesema.

Ameongeza kwamba kulikuwa na mipango ya kumtorosha rais Bazoum kwa kutumia helkopta lakini mipango hiyo imegundulika.

Bw. Bazoum amekuwa chini ya ulinzi nyumbani kwake tangu walinzi wa rais kufanya mapinduzi mwishoni mwa mwezi Julai.

Chapisha Maoni

0 Maoni