Dk. Mwinyi asema Tanzania inatekeleza haki za binadamu na watu

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk. Hussein Mwinyi amesema Tanzania inatekeleza kwa dhati haki za binadamu na watu na kutoa fursa kwa Wananchi wake kupata haki mbalimbali za binadamu na watu.

Dk. Mwingi ameeleza hayo jana akifungua Kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika ukumbi wa kimataifa wa Mikutano AICC Jijini Arusha.

Rais Dk. Mwinyi amesema, Serikali zote mbili zinatekeleza miradi mbalimbali ili kutoa haki za kijamii lakini pia inatoa fursa kwa Wananchi wake kupata haki kwenye vyombo mbalimbali vya sheria.

Aidha Rais Dk. Mwinyi ametolea mfano uhuru wa kupata habari unaotokana na wingi wa vyombo vya habari ambavyo kwa sasa vimepatiwa uhuru wa kufanya kazi zake za kuhabarisha umma bila vikwazo vyovyote.

Chapisha Maoni

0 Maoni