Ndani ya kipindi kifupi cha mwezi mmoja wa Septemba 2023,
Sekta ya Mawasiliano nchini imefanikiwa kuwekeza kiasi cha shilingi za
Kitanzania bilioni 134. Fedha hizi zinawekezwa kwenye Sekta hii muhimu kwa
uchumi wa nchi, ili kuboresha huduma za mawasiliano nchini.
Mafanikio haya makubwa, yametokana na utekelezaji wa maagizo
ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Mheshimiwa Rais, alielekeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari kuhakikisha kuwa inaendelea kuunganisha nchi majirani na
Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
Katika kutekeleza
agizo hilo Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ndani ya Mwezi
Septemba kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania {TTCL} imesaini mikataba ya
kibiashara kati ya Jamhuri ya Malawi na Jamhuri ya Uganda, kufuatia zira za
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu hassan kufanya ziara katika nchi hizo na kukutana
na Marais wa nchi hizo.
Mkataba kati ya Tanzania na Uganda wa kutumia huduma za
Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano una thamani ya Shilingi za Kitanzania bilioni
71.7. Mkataba kati ya Malawi na Tanzania wa kutumia Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano una thamani ya Shilingi za Kitanzania bilioni 13.5. Jumla ya fedha
hizi ni shilingi bilioni 84 za Kitanzania.
Katika hatua nyingine Mhe. Rais aliagiza mgogoro uliodumu
kwa muda mrefu kati ya Serikali na watoa huduma za Mawasiliano nchini utatuliwe
ili kazi ya kuendelea kuboresha huduma za Mawasiliano nchini iendelee kwa kasi
inayotakiwa. Hii ni kulingana na falsafa yake ya Maridhiano, Uvumilivu, Mageuzi
na Kujenga Upya nchi (4R’s - ).
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika
kutekeleza maagizo hayo, mwezi Septemba imekamilisha mazungumzo na watoa huduma
{Consortium of Telecom operators} na kusaini maridhiano na nyongeza ya Mkataba
ambayo thamani yake ni Shilingi za Kitanzania bilioni 50. Aidha, Watoa Huduma
hao wameahidi kuwekeza Shilingi bilioni 32.5 katika maendeleo ya miundombinu
zaidi nchini.
Matukio haua matatu
ndani ya Mwezi mmoja zimevutia Jumla ya kiasi cha shilingi za Kitanzania
bilioni 134 Kwenye Sekta ya Mawasiliano na zingine bilioni 32.5 zitawekezwa na
Makampuni moja kwa moja kwenye Sekta ya Mawasiliano. Haya ni mafanikio makubwa
sana kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Waziri Nape Nnauye katika tukio la kusaini makubaliano
kati ya Tanzania na Uganda alisema anatamani kuona Tanzania inaiunganisha
Afrika kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano nchini. Aidha aliitaka Bodi na
Menejimenti ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL kuhakikisha inatekeleza kwa
ufanisi makubaliano Haya ya kibiashara na hategemei kusikia malalamiko kutoka
kwa nchi hizo mbili.
Haya ni mafanikio makubwa sana kwa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari.
0 Maoni