TLSB yazindua maktaba ya watoto Hospitali ya Sekou Toure

 

Kwa mara ya kwanza, Bodi ya Maktaba ya Tanzania (TLSB), imezindua chumba cha Maktaba ya watoto katika Hospitali ya rufaa ya Sekou Toure, katika Jiji la Mwanza.

Akieleza juu ya azma ya kuchukua hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TLSB Dkt. Mboni Amiri Ruzegea, amesema watoto wanaolazwa Hospitali kwa muda mrefu, huwa wanakosa kmmahali pa kujifunzia na kucheza. Sasa watakuwa wakiitumia maktaba hiyo kwa ajili ya kujifunza.

“Hawapoteza muda. Watakuwa wakitibiwa huku wanajisomea, na kucheza michezo mbalimbali” alisema Dkt. Ruzegea.

Maktaba kuu imetoa vitabu zaidi ya 300, vifaa vya michezo vya watoto, mazulia na picha mbali mbali.

Chapisha Maoni

0 Maoni