Barcelona yampiga mtu 5G ikianza kibabe michuano ya UEFA

 

Barcelona wameanza na ushindi mkubwa katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwa kuichakaza Royal Antwerp magoli matano kwa bila.

Kikosi hicho cha Xavi, walijikuta wakiongoza kwa magoli matatu ndani ya dakika 23, yaliyofungwa na Joao Felix na Robert Lewandowski, pamoja na lakujifunga la Jelle Bataille.

Gavi aliwaongezea Barcelona goli la nne, kabla ya Felix kufunga goli lake la pili katika mchezo huo na kuwafanya waanze vyema michuano hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni