Wananchi wacheni kukimbilia kwa waganga wa jadi- Msigwa

 


Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Gerson Msigwa ameitaka jamii kujenga tabia ya kwenda kupata huduma katika vituo vya afya na kuachana tabia ya kukimbilia kwa wataalam wa tiba asili, jambo linayopelelekea kupotopona na kutumia gharama kubwa.

Bw. Msigwa ameyasema hayo leo Agosti 3, 2023 Jijini Dodoma wakati akiongea kwenye mkutano kati ya waandishi wa habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).

"Kuna baadhi ya watu wakiwa wagonjwa badala ya kwenda kwenye vituo vya afya wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji na huko hawapati tiba stahiki, na kuchelewa kupata matibabu na wengine wanapoteza maisha na baadhi wanatapeliwa kwa kutoa gharama kubwa za kulipia huduma hizo ilihali Serikali imewekeza katika vituo vya afya," amesema Bw. Msigwa.

Pamoja na mambo mengine Bw. Msigwa amewataka watu wanaohusika na kutoa huduma ya tiba mbadala kufuata utaratibu uliopangwa ili kuepusha athari zinazowapata wananchi pale wanapofuata tiba hizo.

Chapisha Maoni

0 Maoni