Wanajeshi watangaza kutwaa madaraka nchini Gabon

 

Maafisa wa Jeshi wamejitokeza kwenye televisheni ya taifa ya Gabon, na kusema kwamba wametwaa madaraka ya nchi hiyo.

Wanajeshi hao wamesema wametengua matokeo ya uchaguzi mkuu wa jumamosi, ambayo yamempa ushindi rais Ali Bongo.

Tume ya uchaguzi ilisema Bongo ameshinda urais kwa chini ya theluthi mbili ya kura zote, katika uchaguzi ambao upinzani wamelalamikia kuwa uligubikwa na udanganyifu.

Kuondolewa madarakani kwa Bongo, kutamaliza utawala wa familia yake kuiongoza Gabon kwa miaka 53.

Gabon ni moja ya mataifa ya Afrika yanayozalisha kwa wingi mafuta, huku asilimia zaidi ya 90 ya ardhi ya taifa hilo ikiwa ni misitu.

Wanajeshi wakitangaza kutwaa madaraka kwenye televisheni ya taifa na kutengua matokeo ya uchaguzi mkuu wa Jumamosi yaliyompa ushindi rais Ali Bongo.

CHANZO: Vyombo vya Kimataifa 

Chapisha Maoni

0 Maoni