Trump ashtakiwa kwa kupanga kubadili matokeo ya urais

 

Aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, ameshtakiwa kwa kupanga kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Trump anakabiliwa na mashtaka manne yakiwamo ya kula njama ya kuiba matokeo, udanganyifu pamoja na uongo.

Mashtaka hayo yanafuatia uchunguzi wa ghasi za kupinga matokeo ya urais huko Washington DC Januari 6, 2021.

Trump anatuhumiwa kusambaza uongo kuhusiana na kufanyika udanganyifu na kuwapo kwa wizi wa kura kwa muda wa miezi miwili.

Kwa ujumla Trump anakabiliwa na kesi tatu za uhalifu, lakini sasa wataalam wa sheria wanasema kesi hii mpya ni ngumu sana kwake.

Chapisha Maoni

0 Maoni