Bei ya petroli na dizeli yapanda, EWURA yatoa sababu

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za

bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano, tarehe 2

Agosti 2023 saa 6:01 usiku. Kwa mwezi Agosti 2023, bei za rejareja za mafuta katika

Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama ifuatavyo:

 

Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Agosti 2023 yanatokana na changamoto za

upatikanaji wa Dola za Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa

thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta

katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta. Bei za mafuta katika miji,

wilaya na mikoa ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 1 na bei za mafuta kwa

wafanyabiashara wa jumla ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 2.

Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei

zinazooneshwa katika Jedwali Na. 1. Aidha, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa

jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 2. Hatua kali

za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili.

EWURA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na

rejareja pamoja na jamii kuzingatia yafuatayo: -

a) bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana kupitia

simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo.

Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa

nchini.

b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za

bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea

kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.

2

c) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya

ushindani isipokuwa bei hizo zisizidi bei kikomo (Price cap) au kuwa chini ya

bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama zilivyokokotolewa kwa mujibu wa Kanuni

za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2023 zilizotangazwa kupitia

Gazeti la Serikali Na. 421 la tarehe 23 Juni 2023.

d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika

mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio vya

kibiashara vinavyotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua,

wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta

kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka

mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa

kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni

husika.

e) Wauzaji wa bidhaa za mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa stakabadhi za mauzo

kutoka kwenye Electronic Fiscal Pump Printers (EFPP) na wanunuzi wahakikishe

wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya

mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hizo zitatumika kama kidhibiti

kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya kuuziwa mafuta kwa

bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora

unaotakiwa. Stakabadhi hizo pia zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za

Serikali zitokanazo na mauzo ya bidhaa za mafuta ya petroli.

Chapisha Maoni

0 Maoni