Shamra shamra za siku ya Simba zahamia Makumbusho ya Taifa

 

Shamra shamra za Wiki ya Simba leo tarehe 4 Agosti 2023 zilihamia Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam baada ya timu hiyo ya mpira wa miguu kuamua kuweka onesho kuhusu historia yao tangu kuanzishwa kwake mwaka 1936.

Onesho hilo lenye vionjo mbalimbali kuhusu timu hiyo limenogeshwa na uwepo kioneshwa cha simba mnyama ambaye amehifadhiwa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ambaye alitolewa na wamasai kwa Mwl. Julius K. Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania kutokana na uongozi bora baada ya kung'atuka mwaka 1985.

Baadhi ya vioneshwa vilivyowekwa kwenye onesho hilo ni pamoja na makombe ambayo timu ya Simba imewahi kupata katika historia ya mchwzo wa mpira wa miguu Tanzania ikiwa ni pamoja na kufika hatua ya fainali katika kombe la Shirikisho la Vilabu barani Afrika (CAF), medali, jezi, picha mbalimbali na bendera.

Oneaho hili lipo wazi jwa wananchi wote wanaotaka kutembelea. Tembelea Makumbusho ya Taifa uione Simba.

Chapisha Maoni

0 Maoni