Muhimbili yamsaidia vifaa mtoto mwenye changamoto ya kupumua

 

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila yamsaidia mtoto mwenye changamoto ya kiafya vifaa vya kumsaidia kupumua.

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na wahisani imemsaidia vifaa tiba mbalimbali mtoto mwenye changamoto ya ukuaji kutokana na kusumbuliwa wa Cerebral Palsy hali inayomlazimu kuhitaji uangalizi wa karibu katika kutatua changamoto za ugonjwa huo.

Mtoto Elisha Kigobanya mwenye umri wa miaka saba alilazwa hospitali hapa takriabni miezi 11 kutokana na tatizo hilo linalomkabili, leo Agosti 15, 2023 ameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupata nafuu.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo kwa wazazi wa Elisha, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Mloganziala Dkt. Julieth Magandi ameeleza kufurahishwa na maendeleo ya kiafya ya mtoto huyo na kuahidi kuwa hospitali itaendelea kuwa bega kwa bega katika kutoa ushauri wa kitabibu pale itakapo hitajika.

"Ni jambo la kushukuru kuona afya ya mtoto Elisha inaendelea kuimarika na sasa ameruhusiwa, nachukua nafasi hii kueleza kwamba pamoja na wahisani wengine kutoa msaada wa godoro hewav (air mattress) pamoja na kitanda uongozi wa hospitali tumempatia msaada wa vifaa vya Oxygen Concentrator na Nebulizer mashine ambavyo atatumia kwa muda mpaka pale atakapokua havihitaji tena, " amesema Dkt.a Magandi

Kwa upande wake Baba mzazi wa Elisha, Bw. Kenneth Kigobanya ameushukru uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa ukarimu, upendo, matibabu na huduma zote za kiutu walizozitoa kwa mtoto wao tangu alipopokelewa hospitalini Septemba 2022.

"Kipekee napenda kuushukru uongozi na watumishi wa Mloganzila kwa namna walivyopambana na kuhakikisha wanaokoa maisha ya mwanangu ambaye awali hali yake kiafya ilikua mbaya,’’ ameeleza Bw. Kigobanya.

@muhimbili_taifa

@elisha_ecpft

Chapisha Maoni

0 Maoni