Filamu ya Barbie yapigwa marufuku Algeria kisa ushoga

Nchi ya Algeria imepiga marufuku filamu maarufu ya Barbie, baada ya wiki tatu tu kupita tangu izinduliwe kwenye taifa hilo lenye Waisalmu wengi la Afrika ya Kaskazini.

Wizara ya Utamaduni ya Algeria imeyataka majumba ya sinema nchini humo kuiondoa mara moja filamu hiyo inayoandaliwa Hollywood, Marekani.

Filamu hiyo inadaiwa kuchochea vitendo ya ushoga, haiendani na imani za dini za Algeria pamoja na mila na tamaduni, maafisa wa nchi hiyo wameliambia shirika la habari la Reuters.

Chapisha Maoni

0 Maoni