Mseminari wa Kanisa Katoliki, Dominiki Melkiori Mahinini, mzaliwa wa Parokia ya Kabanga katika Jimbo la Kigoma, ametekwa nyara na watu wasiojulikana nchini Nigeria, akiwa na Padre Paul Sanoga raia wa Burkina Faso.
Kwa mujibu wa barua ya Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma
Joseph Mlola, viongozi hao wa Kanisa walitekwa nyara na kundi la watu
wasiojulikana mapema usiku wa kuamkia tarehe 03/08/2023 katika Parokia Mt. Luka
Gyenda Jimbo la Minna, nchini Nigeria.
Askofu Mlola ameeeleza katika barua yake hiyo aliyoiandika jana
tarehe 04/08/2023, kwamba Mseminari Dominiki Melkiori Mahinini alikuwa Nigeria
katika mwaka wake wa uchungaji kabla ya kuanza masomo yake ya Teolojia.
Kufuatia tukio hilo Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma kwa
kushirikiana na Mapadre Wamisionari wa Afrika (White Fathers), Askofu Mlola
anawaalika mapadre wote, watawa wote, Waumini Jimbo la Kigomana watu wote wenye
mapenzi mema kusali kuwaombea watumishi hao waliotekwa.
0 Maoni