Marufuku kutumiana nyaraka za Serikali kwenye mitandao ya jamii

 


Serikali kupitia Wizara ya Nchi Menejimenti ya Utumishi Wa Umma na Utawala Bora, imeonya vitendo vya wananchi kutumiana nyaraka za Serikali kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni leo na Naibu Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akijibu swali lililoulizwa na Mhe. Jennyjerry Ntate (Mbunge) wa Viti Maalum.

Akieleza Mhe. Kikwete aliwakumbusha Bunge na wananchi kwa jumla kuwa mawasiliano serikalini yanasimamiwa na sheria na kanuni hivyo ni muhimu kwa wananchi kuzingatia taratibu hizo ili sheria zisiwabane na kuleta taharuki isiyokuwa ya msingi.

Kufuatia kauli hiyo ya Serikali, Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Mwakagendo akataka kujua ni jinsi gani Serikali imejipanga kwenye ujenzi wa mifumo hasa ukizingatia teknolojia ndiyo inakwenda kwa haraka sana.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Kikwete alieleza kuwa wazi imeendelea kujenga mifumo mbalimbali ya Tehama na uwepo wa sheria Namba 10/2019 umewezesha serikali kuwa na uhalali wa uundaji wa mifumo hiyo na hadi sasa mifumo mbalimbali imejengwa kusaidia mawasiliano serikalini na kurahisisha uchapaji kazi.

Chapisha Maoni

0 Maoni