‘Mamba’ Mnangagwa ashinda urais wa Zimbamwe

 

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amechaguliwa muhula wa pili kwa ushindi wa  asilimia 52.6 za kura, tume ya uchaguzi ya nchi hiyo imesema.

Hata hivyo upinzani nao umedai kushinda uchaguzi huo, ukisema kumekuwapo na udanganyifu mkubwa wa kura, huku waangalizi wakisema uchaguzi huo haukukidhi viwango vya demokrasia.

Mnangagwa maarufu kwa jina la Mamba ni rais wa tatu wa nchi hiyo, ambaye aliingia madarakani mwaka 2017 kufuatia mapinduzi dhidi ya Robert Mugabe.

Wananchi wa Zimbabwe bado wanakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei, umasikini pamoja na hofu ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Chapisha Maoni

0 Maoni