Chelsea yavunja rekodi ya kutoa paundi milioni 115 kumnasa Caicedo

 

Timu ya Chelsea imeridhia kunasa saini ya kiungo wa Brighton, Moises Caicedo, kwa kiwango cha ada ya uhamisho iliyovunja rekodi Uingereza ya paundi milioni 115.

Timu ya Liverpool nayo iliweka dau la ada ya paundi milioni 111 Ijumaa kwa mchezaji huyo raia wa Ecuador mwenye umri wa miaka 21.

Hata hivyo Caicedo aliichagua Chelsea na hatimae wamefanikiwa kumnasa kwa dau hilo jipya baada dau lao la awali kukataliwa na timu ya Brighton kipindi hiki cha majira ya joto.

Kwa dau hilo inamaana Chelsea itavunja rekodi ya Uingereza ya uhamisho mara mbili mwaka 2023, baada ya kumnunua kiungo Muargentina Enzo Frenandez kwa paundi milioni 107, Januari.

Chapisha Maoni

0 Maoni