Ali Bongo ayaomba mataifa rafiki yapaze sauti zao baada ya kupinduliwa

 

Rais Ali Bongo ameonekaka kwa mara ya kwanza kwenye video aliyotuma tangu kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi Gabon, akiwaomba marafiki wa nchi hiyo duniani kote kupaza sauti zao kupinga mapinduzi.

Ali ambaye alikuwa akionekana kama mtu ambaye si rahisi kutetereka ama kutetemeshwa ameonekana akiwa mnyonge na mpweke.

Katika video hiyo Ali Bongo amesema kuwa anashikiliwa katika makazi yake, hayupo na mkewe na mtoto wake pia yupo kwingine.

“Sijui kinachoendelea nimeshikiliwa kwenye makazi yangu, nawaomba marafiki wote tulionao duniani mpaze sauti zenu dhidi ya hiki kinachoendelea, nawaomba mpaze sauti,” Ali amesema kwenye video hiyo.

Jeshi la nchi hiyo limetangaza kutengua matokeo ya uchaguzi wa rais ya Jumamosi yaliyompa ushindi rais Ali Bongo, na kuunda kamati ya mpito ya mabadiliko ya utawala wa nchi hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni