Waziri Bashe ataka nchi za SADC kushirikiana chakula


 Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ametoa rai kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kushirikiana kuzalisha chakula kwa mpango ambao kila nchi itanufaika.

Mhe. Bashe ameyasema hayo leo tarehe 3 Julai, 2023 alipowasilisha mada kuhusu Kilimo cha Kiisasa kama njia ya kukabiliana na upungufu wa chakula katika mkutano wa 53 wa Mabunge ya SADC (SADC PF 53) unaofanyika jiji Arusha.


 Waziri Bashe amesisitiza kuwa  kila nchi izalishe mazao ambayo itawauzia  wengine kutokana kwa kutegemea  uwezo  wa nchi husika wa  kuzalisha zao husika.


Ametoa mfano wa uwezo wa Tanzania katika kuzalisha mahindi na mchele ukilinganisha na nchi nyingine za SADC na kusema ni vema nchi nyingine zinunue chakula hicho na Tanzania inunue mazao mengine kutoka nchi za wanachama.


Waziri Bashe ameongeza kuwa kwa sasa tishio kubwa linalozikabili nchi nyingi za SADC ukiondoa Afrika Kusini ni upatikanaji wa mbegu,  jambo ambalo linaweza kukwamisha jitihada za kuwa na uhakika wa chakula.


Kuhusu njia za kisasa za kuendesha kilimo, Waziri Bashe amesema Tanzania imepanga kuwa na hekta za mrabam ilioni nane za kilimo cha umwagiliaji ifikapo mwaka 2030 ili kujiwekea uhakika wa kuzalisha chakula kipindi chote cha mwaka.

Chapisha Maoni

0 Maoni