Wamiliki wa magari wasisitizwa kutumia mfumo wa gesi

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba wananchi wenye magari kugeukia mfumo wa nishati ya gesi kwa kufunga kwenye magari yao kwa kuwa unapunguza gharama kwa asilimia 40 ukilinganisha na Dizel na Petroli.

Mhandisi Felchesmi Mramba ametoa wito huo katika mdahalo ulioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), kuhusu mafuta na gesi asilia ambapo amesema utafiti uliofanyika unaonyesha matumzii ya nishati ya gesi kwenye  magari unapunguza garama kwa asilimia 40 ukilinganisha na  dezeli na petroli.


Amesema serikali inakaribisha sekta binafsi ziweze kushiriki katika kujenga vituo vya kusambaza gesi kwenye magari na  kuanzisha karakana ya kubadilisha magari yanayotumia mafuta na gesi kwa pamoja.


Amesema lengo ni kuona wananchi wengi wanatumia magari yenye mfumo wa gesi. Hivyo hivyo kwa majumbani gharama yake iwe  chini Tanzania inakadiriwa kuwa na mita trilioni 230 za ujazo za gesi asilia, ingawa zilizothibitishwa mpaka sasa ni futi trilioni 57.5, hivyo kuiweka kwenye ramani ya dunia ikishika nafasi ya 82.

Chapisha Maoni

0 Maoni