Wawekezaji wawili kutoka Urusi wakiambatana na Mwenyekiti wa
bodi ya Wakurugenzi ya TAWA Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko wametembelea
banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika maonesho ya 47 ya kimataifa ya
kibiashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam na kupata maelezo juu ya fursa za
uwekezaji zinazopatikana katika maeneo ya mapori ya akiba na mapori tengefu
nchini.
Wawekezaji hao wameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Kwa juhudi za kuhifadhi Wanyamapori nchini
Kwa nyakati tofauti wakiwa katika bustani ya Wanyamapori hapo
jana waliweza kuona Wanyamapori hai mbalimbali kama vile Simba, chui, chatu,
mbuni na wengine wengi waliopo katika bustani hiyo na kupongeza juhudi za
Serikali katika kuwalinda na kuwahifadhi Wanyama hao kwa ajili ya urithi wa
vizazi vijavyo
"Tumetembelea bustani ya Wanyamapori na kuona aina
mbalimbali za Wanyama mahali hapa tumefurahi sana, hakika mnatoa viwango vya
juu vya huduma Kwa Wanyamapori hawa na tunawaona watu wengi wakifurahi kuwaona
Wanyamapori" amesema mmoja wa watalii hao
"Nimependa pia kuona namna mnavyowaleta Wanyamapori
karibu na watu wenu Ili waweze kuwaona kirahisi, hii inaonesha tangu utoto watu
wenu wanajifunza uhifadhi, hongereni sana na tunawatakia Kila lakheri"
ameongeza
Wawekezaji hao wamekuja Nchini Kwa lengo la kutaka kuwekeza
katika maeneo mbalimbali yanayosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori
Tanzania (TAWA).
0 Maoni