Watu wapatao 44 wamekufa baada ya kutokea mlipuko nchini
Pakistani, wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na chama cha Kiislam.
Zaidi ya watu 100 pia wamejeruhiwa katika mlipuko huo
uliotokea kaskazini-magharibi mwa Wilaya ya Bajaur ambapo chama cha Jamiat
Ulema-e-Islam-Fazl (JUI-F) kilifanya mkutano wake.
Polisi wameiambia BBC kwamba wamebaini ushahidi kuwa mlipuko
huo ulitokana na mtu anayedaiwa kujilipua kujitoa mhanga.
Zoezi la uokoaji limekamilika na watu wote waliojeruhiwa
wamepelekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
0 Maoni