OFISI ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
kupitia Idara ya Kazi imewataka waajiri wa sekta binafsi nchini kuzingatia kima
kipya cha chini cha mshahara kilichotangazwa na serikali mwaka huu kwa kuwa ni
takwa la kisheria.
Kima hicho kilitangazwa katika kupitia tangazo la serikali
namba 687 na kilianza kutumia Januari mosi, 2023 na kimewekwa kwenye sekta kuu
13.
Kamishna wa Kazi Msaidizi, Mahusiano kazini wa Ofisi hiyo,
Andrew Mwalwisi ameyasema hayo Julai 19, 2023 alipokuwa akitoa elimu kwa umma
jijini Dodoma kuhusu sheria na miongozo ya kazi.
Amesema kwa sekta ya kilimo ni Sh.140,000, afya
(Sh.195,000), mawasiliano imegawanyika kuna sekta ya huduma za mawasiliano
(Sh.500,000), huduma za utangazaji na vyombo vya habari, posta usafirishaji vifurushi
ni (Sh.225,000) kwa anayeanzia chini kabisa.
“Kazi za majumbani imekuwa changamoto kidogo ya kutoelewa
kwa majumbani hii sekta imegawanyika kwenye makundi manne kuna wafanyakazi wa
kazi za ndani walioajiriwa na wanadiplomasia na wafanyabiashara wakubwa
wanapaswa kulipwa Sh. 250,000, kuna walioajiriwa na Maafisa wenye stahiki Sh.
200,000, kuna wanaoishi katika kaya ya mwajiri hawa ndo wengi ndo wengi
wanapaswa kulipwa Sh. 120,000 na wanaokwenda na kurudi Sh.60,000,” amesema.
Alibainisha hoteli kubwa za kitalii kima cha chini ni
Sh.300,000, za kati Sh. 180,000, migahawa, nyumba za kulala wageni na baa Sh.
150,000, ulinzi binafsi (kwa kampuni kubwa Sh.220,000 na madogo ni Sh.
148,000), sekta ya nishati (kampuni za kimataifa 592,000 na madogo ni Sh. 225,000),
Usafirishaji (wa anga Sh. 390,000, utoaji mizigo na usambazaji Sh.360,000, nchi
kavu kwa madereva wao wanapaswa kima cha chini kiwe Sh. 300,000 kwa mwezi.
“Kuna sekta ya ujenzi (daraja la kwanza Sh. 400,000, la pili
hadi la nne sh.360,000, la tano hadi la saba Sh. 320,000), sekta ya madini (uchimbaji na utafutaji
madini Sh. 500,000, wenye leseni za wachimbaji wadogo sh. 300,000, biashara
sh.450,000, madalali sh. 250,000), huduma za shule binafsi ni Sh. 207,000, sekta ya biashara na viwanda Sh.150,000,
taasisi za fedha Sh. 592,000, uvuvi na huduma ya baharini sh.238,000 na sekta
nyinginezo ambazo hazijatajwa kwenye makundi hayo ni Sh. 150,000 kwa mwezi,”
amesema.
0 Maoni